RIZIKI ALMAS

Position: Senior Diamond leader
Phone: +255656357443
Categories: Car Awards, Top Leader, Travel Awards

SAFARI YANGU YA MAFANIKIO NDANI YA KAMPUNI YA BFSUMA.

Naitwa Riziki Almas, ni mama wa watoto wawili, nimemaliza chuo kikuu Cha dar es salaam mwaka 2014, na sikufanikiwa kupata ajira,hivyo nilijiari na kufungua ofisi ya ushonanji nguo, kutokana  na changamoto za biashara ( Kodi, ujuzi, rasiliamali watu) nilishindwa kuendelea na kufunga ofisi yangu ya ushonaji , na ndio nilipokutana na fursa hii ya biashara ( BFSUMA) kupitia rafiki yangu nilosoma naye chuo Iman mosses Mwasaka, Kwa Sasa ni mjasiriamali mkubwa kupitia kampuni ya BFSUMA niliyeanza safari yangu ya mafanikio mnamo 29/01/2016 na ninashukuru Mungu Kwa kuwa imenisaidia kutimiza ndoto zangu nilizokua naona siwezi kutimiza kabla sijaanza biashara.

Ndoto kubwa nilonayo ndio ilikuwa chachu ya kuchagua kampuni ya BFSUMA. ndoto yangu ni kuwasaidia watu zaidi ya 1000 kutimiza ndoto zao na kuziishi  mpaka 2025 hii ndoto itakuwa imetimia na Pili kuwa na kampuni ya uwekezaji wa makazi na viwanja( real estate) mpaka mwezi 12/2026 ndoto yangu hii itakuwa imetimia.

MAFANIKIO NILOPATA MPAKA SASA 2022

SAFARI

Nimefanikiwa kupata tuzo za safari ndani ya bara la afrika na Asia ( intercontinental travel awards) na safari za kimataifa (international travel awards) mpaka sasa nimeweza kwenda nchi 4 ikiwepo Thailand,Hongkong, south Africa, Kenya.

GARI

Nimefanikiwa kushinda tuzo ya Gari( Normal car award) 2022 aina ya Audi A4 yenye thamani ya Dola 12,500 za kimarekani na nimeweza.

BONUS KUBWA

Nimefanikiwa kuwa miongoni mwa watu wanaopokea Malipo makubwa( bonus) kubwa ndani ya kampuni yaani ni miongoni wa kumi Bora wanaopokea bonus kubwa ndani ya Tanzania.

HARAKATI ZA WANAWAKE(AMBITIOUS WOMEN)

Nimefanikiwa kuanzisha harakati za wanawake walioamua kupambania NDOTO zao, tunakusaidia kutambua uwezo/nguvu ulionao kiasili katika kujenga JAMII yenye mafanikio makubwa bila kutelekeza NDOTO zako. Kama wewe ni mpenda harakati hizi ungana nami kwenye kurejesha furaha na uwezo wa Mwanamke.

TIMU KUBWA ( BRIGHTER TEAM)

Nimefanikiwa kujenga biashara yangu kubwa Tanzania bara na visiwani na  imenisaidia kuwafikia vijana,wazee na watanzania wengi wenye njaa ya Mafanikio bila kujali elimu zao, historia zao,ujuzi wao Hivyo hata wewe unayesoma hii waweza jiunga Kwa timu yangu ili ufikie “NDOTO YAKO KUBWA ULOTELEKEZA.”
Mimi nakwambia inawezekana kunyanyuka Tena na KUPIGANIA NDOTO yako.

© 2024 MPANGO MZIMA. All Rights Reserved