EVA NICODEMAS MTEKELE
Kwa jina naitwa Eva Nicodemas Mtekele, ni kiongozi ngazi ya 7 katika kampuni ya BF SUMA.
Katika kuzifikia ndoto, kila mmoja ana story yake, ndefu na nyingine huwa hazina mwisho.
Kwa ufupi, yangu inaanzia nilipotamani kuziishi ndoto zangu za kutoa huduma ya afya na kuwa na mafanikio makubwa.
Kwa wakati ule, haikuonekana wazi sana..njia ilikuwa na vumbi la majukumu na upepo wa presha za kuwa mama wa vijana watatu. Ashukuriwe Mungu baada ya kujiunga na kampuni ya BF SUMA, nimeanza kuona mwanga wa mafanikio si tu kwa kutoa huduma tu, bali pia kwa kugusa maisha ya watu kiuchumi na kwa kila mmoja anayepona kutokana na bidhaa na maelekezo sahihi ninayoyatoa kupitia Eva Health Service, chini ya BF SUMA